Suala linalohusiana na wingi wa makundi linahitaji kuandikiwa kitabu ili watu wajue wale ambao wanajuzisha uwepo wa makundi mengi kama mfano wa Yuusuf al-Qaradhwaawiy, ´Abdul-Wahhaab ad-Daylamiy, Swalaah as-Saawiy na ´Aqiyl al-Matrafiy kwamba wanalingania katika kudangana. Ni lazima wapatikane wanafunzi wataochukua jukumu hili la kuandika kitabu kilicho na Hadiyth na Aayah za Qur-aan ili kuwafichulia watu hali za watu hawa.

Kuhusu Swalaah as-Saawiy ni mwenye kuchukua nafasi ya Sa´iyd Hawwaa. Wewe, Swaalih as-Saawiy, utakufa kama vilivyokufa vitabu na fikira zako. Hivo ndivo alivokufa Sa´iyd al-Hawwaa, vitabu vyake na fikira zake. Najua kwamba ulikuwa mtu mzuri wakati ulipokuja Misri. Nakuonya kufa katika hali hiyo. Unaita katika kufarikisha na kutenganisha umoja wa waislamu na kutekeleza njama za Marekani. Marekani inataka tubaki tukiwa ni wenye kutengana na kugawanyika.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-ih wa Naswaa-ih, uk. 102
  • Imechapishwa: 12/04/2020