Watoto kujifanyia ´Aqiyqah wao wenyewe ikiwa baba hakufanya

Swali: Kuna mtu ana watoto sita na hakumfanyia ´Aqiyqah isipokuwa mmoja tu katika wao. Ni ipi hukumu? Ni lipi la wajibu kwake? Je, ni wajibu kwa watoto kujifanyia wao wenyewe ´Aqiyqah pamoja na kuzingatia ya kwamba watatu katika wao wana uwezo juu ya hilo?

Jibu: Ikiwa baba huyu ambaye hakuwafanyia ´Aqiyqah watoto wake wote hawa ni fakiri hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu ´Aqiyqah ni kama mfano wa zakaah. Kama ambavo fakiri halazimiki zakaah kadhalika fakiri halazimiki vilevile ´Aqiyqah.

Lakini kama alikuwa ni tajiri lakini kila siku anasema kwamba atafanya kesho kesho, katika hali hii tunamwambia kwamba awafanyie ´Aqiyqah watoto wake ambao hakuwafanyia. Wakitaka baadhi yao kujifanyia wao wenyewe, basi wapate kwanza idhini kutoka kwa baba yao na wamweleze kwamba wanataka kujifanyia wao wenyewe. Kwa sababu jukumu la ´Aqiyqah ni la baba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1008
  • Imechapishwa: 19/01/2019