Swali: Je, msemo huu ni sahihi: “Kiongozi ni yule ambaye amepewa bay´ah na Waislamu wote duniani, kuanzia mashariki mpaka magharibi”?

Jibu: Haya ni maneno ya Khawaarij. Kiongozi ni yule ambaye amepewa bay´ah na Ahl-ul-Hall wal-´Aqd katika Waislamu. Ni lazima kwa waliobaki kumtii. Sio lazima wote, kuanzia mashariki mpaka magharibi, wanaume kwa wanawake, kumpa bay´ah. Huu sio mfumo wa Uislamu katika kumteua kiongozi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_14.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2018