Watakeni ushauri kina mama kabla ya ndoa


Nilimwandikia Abu ´Abdillaah:

“Mtoto wa dada yangu amemposa msichana wa kaka yangu na mama yake hataki.” Akajibu: “Usifanye hivo.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watakeni ushauri wanawake juu ya wasichana zao.”

Kuhusu ufukara, unapaswa kumuoza kwa hali yoyote. Ufukara na utajiri unatoka kwa Allaah.”[1]

Nikamuoza fukara huyo na sikuona isipokuwa kheri tupu.

[1] Abu Daawuud (2095). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhaw´iyfah” (3/677).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Abiy Harb al-Jarjaara’iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 83
  • Imechapishwa: 16/03/2021