Waswaliji wenye kuona imamu amezidisha na wengine hawaoni hivo

Swali: Imamu alisimama katika Rak´ah ya tano katika swalah ya Rak´ah nne. Maamuma baadhi yao wana shaka na wengine wana uhakika. Lakini wote wakasimama pamoja naye.

Jibu: Ambaye ana shaka atasimama. Ambaye ana uhakika anatakiwa kusema:

سبحان الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

سبحان الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

na asisimame.

Swali: Ambaye amefanya kwa kukusudia anatakiwa kuirudi swalah yake?

Jibu: Hapana, hakuna kinachomlazimu muda wa kuwa ni mjinga na hajui hukumu ya ki-Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21682/حكم-من-قام-مع-الامام-لخامسة-لشك-او-جهل
  • Imechapishwa: 11/09/2022