Waswaliji wameswali nyuma yake pasina imamu kujua

Swali: Nilikuwa naswali sunnah ya baada ya Dhuhr. Tahamaki kundi la watu likajiunga na mimi na likanifanya kuwa ni imamu wao ambapo wakaswali nyuma yangu. Sikuweza kufanya kitu ambapo nikakamilisha swalah yangu pamoja na kuzingatia ya kwamba sikunyanyua sauti wakati wa Takbiyr na Tasliym. Pamoja na hivo wakakamilisha swalah zao nyuma yangu ambapo  wakasimama na kuswali Rakaa´ mbili. Hata hivyo nilipuuzia kuwafahamisha kwa sababu baada ya Takbiyr nilisimama na kwenda zangu. Ni ipi hukumu ya swalah yangu na swalah zao?

Jibu: Ikiwa ulinuia uimamu swalah zao zinasihi. Ama ikiwa hukunuia uimamu na bado ukaendelea kunuia kuswali peke yako, lililo salama zaidi ni wao kuzirudi swalah zao. Lakini ikiwa waliswali nyuma yake na akanuia uimamu na wao wakamfuata swalah zao zinasihi kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaswali peke yake halafu akaja Ibn ´Abbaas na kuswali nyuma yake ambapo wakawa mkusanyiko. Makusudio ni kwamba ikiwa amenuia uimamu swalah zao zinasihi. Ama ikiwa hakunuia basi lililo salama zaidi ni wao kurudi kuswali tena.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2018