Waswaliji hawakumfuata imamu katika Rak´ah ya tano aliyosahau al-Faatihah

Swali: Imamu akisahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah ya nne kisha akakumbuka kabla ya Tashahhud ya mwisho ambapo akasimama kwa ajili aweze kusoma al-Faatihah. Maamuma nyuma yake wakasema “Subhaan Allaah” lakini hata hivyo hakurudi na maimamu hawakumfuata kwa kudhania kwao kwamba ni Rak´ah ya tano. Baada ya hapo imamu akawabainishia waswaliji hali halisi. Je, wanatakiwa kuiswali Rak´ah hiyo?

Jibu: Udhahiri ni kwamba wanatakiwa kuiswali. Lakini [imamu] alikuwa anatakiwa awaashirie kwa mkono wake au awawekee wazi kitu kitachowafahamisha hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 07/05/2019