Swali: Nini hukumu ya kile kinachofanywa na baadhi ya watu wanawaagiza baadhi ya watu [walete] nguo au kanzu. Watu hawa wanadai baada ya hapo wanajua ni magonjwa yepi na dawa ipi itayofaa.

Jibu: Ni haramu kwenda kwa wenye kudai kujua mambo yaliyofichikana. Haijuzu kuwapelekea nguo na kanzu wala kitu kingine. Ni haramu kuwasadikisha kwa wanayoyasema. Kuna Hadiyth Swahiyh zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazotolea dalili juu ya hilo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/417)
  • Imechapishwa: 24/08/2020