Swali: Wakati ninapotawadha na katikati ya wudhuu´ huhisi kama kuna kitu kinachonitoka kwenye uume wangu. Je, hiyo ina maana kwamba nimenajisika? Je, nikihisi kutoka kwake wakati niko naswali swalah yangu inabatilika?

Jibu: Mswaliji kuhisi kitu kinatoka kwenye tupu yake ya nyuma au ya mbele hakuchengui wudhuu´ wake na wala asijali hisia hizo. Hiyo ni wasiwasi wa shaytwaan.  Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliulizwa mfano wa jambo hilo ambapo akasema:

“Asiondoke mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Lakini mswaliji akiwa na uhakika kiyakini kabisa wa kutokwa na upepo, mkojo na mfano wake basi swalah yake inabatilika kwa sababu twahara yake imeharibika. Hivyo atalazimika kurudia kutawadha na kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/126)
  • Imechapishwa: 21/08/2021