Swali: Ni ipi hukumu ya kunyoa ndevu katika nchi ambayo wanamshinikiza kila ambaye anafuga ndevu zake kwa hoja kwamba eti ni katika wenye msimamo mkali?

Jibu: Hizi ni dhana za nafsi. Haifai kwake kunyoa ndevu zake kwa sababu ya kuwaogopa watawala. Bali ni lazima kwake kumcha Allaah. Afuge na arefushe ndevu zake. Yuko na kiigizo chema na usalama endapo atanyooka na kuwa mkweli. Asiwaingilie katika kazi zao. Hatoona katika hali zake, biashara zake na kumtii kwake Mola wake isipokuwa kheri tupu.

Wakimtenza nguvu na wakamnyoa hakitomdhuru kitu hicho. Dhambi zitawapata wao. Lakini yeye kunyoa kwa sababu eti wasimkamate, huo ni wasiwasi na upotofu wa shaytwaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2672/حكم-حلق-اللحية-بسبب-الضغط-والاضطهاد
  • Imechapishwa: 28/03/2021