Wasiwasi ndani ya swalah na namna ya kujikwamua nao

Swali: Mimi ni kijana ambaye kila ninapoingia ndani ya swalah basi shaytwaan ananitia wasiwasi; naanza kufikiria kwamba nimepatwa na jini. Siku zote natafuta mtu wa kunisomea na hufikiria mambo ambayo ni muhali yatokee. Je, kuna Dhikr niwezayo kusoma kuniondoshea jambo hilo?

Jibu: Dhikr ni kitu kipo na himdi zote ni za Allaah. Kila ugonjwa una dawa yake. Mashaytwaan na majini sio walimwengu wenye kuonekana ambao mtu anaweza kujilinda nao kwa kutumia silaha au kwa wanajeshi. Ni walimwengu wasioonekana ambao humvamia yule ambaye halazimiani na nyuradi. Kwa ajili hiyo nawahimiza kufanya nyuradi kwa wingi na kudhukuru kwa wingi ili muweze kusalimika adhabu za watu hawa.

Namnasihi ndugu huyu amdhukuru Allaah (´Azza wa Jall) kwa wingi, kusoma Qur-aan na aombe ulinzi dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa. Akihisi kitu na akadhania kwamba jini kamwingilia, aiulize nafsi yake ni vipi jini litaweza kumwingilia halafu amwombe Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa. Ajisubirishe na astahamili. Pamoja na Dhikr na Qur-aan yatamwondoka kwa nguvu za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1033
  • Imechapishwa: 23/02/2019