Wasioswali wanatakiwa kushtakiwa

Swali: Kuna watu wanafikisha miaka 24 na 25 lakini hata hivyo hawaswali.

Jibu: Hawa wanatakiwa kwenda kushtakiwa kwa watawala au mahakamani. Ikithibiti kweli kwamba hawaswali basi wanatakiwa kuambiwa watubie na vinginevyo wauawe. Tunamuomba Allaah afya. Akiacha kuswali na huku anakanusha kuiacha anakuwa kafiri na murtadi. Ama ikiwa ni mtu anayechukulia wepesi na wakati huohuo anaamini kuwa ni wajibu hapa ndipo wanachuoni wametofautiana. Maoni ya sawa ni kwamba anakufuru vilevile. Akiacha kuswali, ijapokuwa atakuwa ni mwenye kuacha uwajibu wake, ni kafiri. Haya ndio yamenukuliwa kutoka kwa Maswahabah ambao wameafikiana juu ya ukafiri wake. ´Abdullaah bin Shaqiyq al-´Uqayliy, Ishaaq bin Raahuuyah, Ibn Hazm na wengineo wamenukuu hivo. Baadhi ya wanachuoni waliokuja nyuma wanaonelea kuwa ni kufuru ndogo. Maoni ya sawa ni kwamba ni kufuru kubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2018