Wasikilizaji Qur-aan wanapata rehema za Allaah

Swali: Je, ni kweli mwenye kumsikiliza msomaji Qur-aan anapata ujira sawa na yule mwenye kusoma?

Jibu: Hapana, anapata thawabu za kusikiliza. Allaah (´Azza wa ´Alaa) amesema:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Inaposomwa Qur-aan basi isikilizeni na nyamazeni kimya ili mpate kurehemewa.” (07:204)

Anapata huruma wa Allaah (´Azza wa Jall) na analipwa thawabu kwa ajili ya hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17477
  • Imechapishwa: 25/11/2017