Swali: Mimi ni mwalimu wa kike katika shule ya msingi ambapo nawafunza mada ya Qur-aan wanafunzi wa kike wa darasa la pili. Wanafunzi hawa ni wadogo na hawajui vizuri kutia wudhuu´ na pengine wasijali jambo hilo. Hugusa pasi na wudhuu´ Qur-aan na kunifuata. Je, napata dhambi kwa jambo hilo baada ya kuwawekea wazi namna ya kutawadha na wakatambua?

Jibu: Wakiwa ni wasichana wa miaka saba basi ni lazima kuwafunza wudhuu´ hadi wajue. Baada ya hapo wanaweza kugusa msahafu. Wakiwa chini ya hapo wudhuu´ kwao hausihi na wudhuu´ si katika shani yao. Hata hivyo waandikiwe kwenye ubao au karatasi na wasiguse msahafu na hilo litatosha – Allaah akitaka. Wajitahidi katika jambo hilo. Ni jukumu kwako kuwaelekeza, kuwaongoza na kuwafunza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/146)
  • Imechapishwa: 23/08/2021