Wasia wa mzee ambaye mara nyingine anatokwa na akili

Swali: Bibi yangu ni mtumzima sana na yuko na mali. Ametoa wasia wa kujengewa msikiti pamoja na kuzingatia ya kwamba wakati fulani anaswali, mara anatujua na anayatambua mambo mengi na wakati mwingine hajui. Bibi huyu ana msichana, ambaye ni mama yangu, na mama huyu ana wajukuu ambao ni watoto wa khali yangu aliyefariki. Mali hiyo niko nayo mimi. Je, niitumie kwa kutengeneza msikiti kama vile alivousia au nizifanye nini? Nikifikiwa na kifo nifanye nini?

Jibu: Allaah akimkadiria akafa kabla ya kutekeleza wasia, mali hiyo inarudi kwa warithi. Katika hali hiyo wakitaka kujenga msikiti ni sawa na Allaah atawajaza kheri. Kuhusu kabla hajafa haijuzu kwake kuzitumia atakavyo. Kwa sababu mzee huyu maneno yake hayana hukumu yoyote kwa sababu hahisi na wala hajui anachokisema. Maneno yake hayana maana yoyote na wala haijuzu kutekeleza kitu katika yale aliyoyasema. Isipokuwa pale atapokuwa amesema kwa uelewa na fahamu, ndio [utatekelezwa wasia wake].

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1581
  • Imechapishwa: 17/10/2018