Wasafiri kuswali swalah ya ´Ishaa nyuma ya imamu anayeswali Maghrib


Swali: Kundi la wasafiri likiingia msikitini na wakakuta watu wanaswali swalah ya Maghrib baada ya kuwa wao wamekwishaswali. Je, inajuzu kwao kuswali Rak´ah mbili na kuketi na kutoa Tasliym au wafanye nini?

Jibu: Jambo hili linahitajia kanuni; msafiri akijiunga na imamu ambaye ni mkazi basi ni wajibu kwake kukamilisha swalah yake. Haijalishi kitu hata kama hakuwahi isipokuwa tu Tashahhud ya mwisho. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kile mtachowahi kiswalini na kile kitachokupiteni basi kikamilisheni.”

Hakupambanua.

´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliulizwa kuhusu mtu ambaye ni msafiri kuswali Rak´ah mbili pamoja na imamu Rak´ah nne ambapo akajibu kwamba hiyo ndio Sunnah.

Kwa hivyo ni wajibu kwa msafiri akijiunga na imamu ambaye anaswali kikamilifu akamilishe swalah yake. Lakini wakati mwingine mtu anafika kwenye uwanja wa ndege na anawakuta watu wanaswali na huku hajui kama wanaswali kikamilifu au wanafupisha. Katika hali hii afanye nini? Hakujiunga nao tokea  mwanzoni wa swalah, kwani angelifanya hivo basi angejua hali yao. Katika hali hii afanye nini? Hapa anatakiwa atazame; ikiwa imamu ana alama za safari kwa mfano ana begi pembezoni mwake na mavazi ya safari, basi achukue ule uinje juu ya kwamba imamu atafupisha. Lakini akiwa na alama za ukazi kama kwa mfano imamu huyo ni mfanyakazi wa hapo uwanja wa ndege ambapo wanakuwa na mavazi maalum, katika hali hii anuie kukamilisha kwa sababu udhahiri ni kwamba atakamilisha swalah. Kwa hiyo atende kwa mujibu wa ule udhahiri. Akiwa bado yuko na mashaka na asibainikiwe, basi katika hali hii tunasema akichukulia salama zaidi na akakamilisha ndio bora zaidi. Endapo atafupisha pia hakuna neno.

Swali: Kundi la wasafiri likiingia msikitini na wakakuta watu wanaswali swalah ya Maghrib baada ya kuwa wao wamekwishaswali. Je, inajuzu kwao kuswali Rak´ah mbili na kuketi na kutoa Tasliym au wafanye nini?

Jibu: Wakijiunga na ambaye anaswali Maghrib na bado hawajaswali ´Ishaa, lililo la wajibu kwao ni kumfuata imamu. Imamu aitoa Tasliym wanatakiwa kuswali Rak´ah ya nne. Mtu pia anaweza kusema kwamba si lazima kwao kumfuata katika ile Rak´ah ya nne kwa sababu imamu anaswali swalah isiyokuwa na Rak´ah nne, anaswali swalah yenye Rak´ah tatu, hivyo wanaweza kukaa baada ya Tashahhud ya kwanza, halafu wamsubiri imamu na watoe Tasliym pamoja naye. Kwa sababu wao swalah yao ni ya ´Ishaa na swalah ya imamu ni Maghrib. Lakini lililo bora ni wao kumfuata na akitoa Tasliym wakamilishe Rak´ah ya nne.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1075
  • Imechapishwa: 25/03/2019