Jambo la pili inatakiwa kurejea kwa wanachuoni walezi ambao wanatendea kazi Kitabu cha Allaah na wanakilinda kutokamana na upotoshaji wa wenye kuchupa mpaka, uongo wa watu wa batili na tafsiri mbovu za wajinga. Tunatakiwa kuwafungamanisha watoto na vijana wetu kwa wanachuoni hawa. Tunatakiwa kuwahimiza kusoma kwao na kuchuma faida kutoka katika darsa zao. Kwa sababu elimu ni kwa kujifunza na upole ni kwa kuufanyia mazoezi. ´Umar na bwana mmoja katika Answaar (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakipeana zamu kwenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakielezana walichojifunza. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Na haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [kupigana vita vya jihaad]. Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi [moja] wajifunze dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا

“Linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wale wenye madaraka kati yao basi wale wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua.Lau si fadhila za Allaah juu yenu na rehema Zake basi hakika mngelimfuata shaytwaan isipokuwa wachache tu.” (04:83)

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=ZgvvTeINWa0
  • Imechapishwa: 19/03/2021