Swali: Miongoni mwa wanaostahiki kupewa zakaah ni wale waliotajwa katika maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ
“… na katika njia ya Allaah.”[1]
Je, makusudio ni wale wapiganaji peke yao au wanaingia hata wale wanaolingania na wengineo?
Jibu: Makusudio ni wale wapiganaji peke yao; wapiganaji wenye kujitolea ambao hawapati mishahara kutoka serikalini.
[1] 09:60
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (64) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%2019-03-1438H.mp3%2001.mp3
- Imechapishwa: 09/10/2017