Swali: Mikono inawekwa wapi katika swalah? Ni kwenye kifua au chini ya kitovu? Kuna Hadiyth yoyote Swahiyh kuhusu hilo?

Jibu: Inajuzu kuweka mikono juu ya kifua na chini ya kitovu. Kuna dalili kwa yote mawili. Ijapokuwa dalili ya kuweka juu ya kifua ndio sahihi zaidi. Hivyo imekokotezwa zaidi kuiweka juu ya kifua. Inajuzu kwake kuiweka chini ya kitovu. Yote mawili yanajuzu, lakini lililo bora zaidi ni kuiweka kwenye kifua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 28/05/2018