Wapi anapotazama mwenye kuomba du´aa ndani ya swalah?

Swali: Katika du´aa ya Qunuut mswaliji hunyanyua mikono yake. Ni wapi hutazama? Je, atazame kwa juu au atazame sehemu anaposujudia?

Jibu: Kuhusu kunyanyua macho yake mbinguni haijuzu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kwa yule mwenye kuswali kunyanyua macho yake mbinguni na akazungumza hilo kwa ukali pale aliposema:

“Watu wataacha kufanya hivo au yatapokonywa macho yao.”

Hii ni adhabu kwao. Hapana shaka kwamba mtu kunyanyua macho yake mbinguni kunapingana na kuwa na adabu kwa Allaah. Kwa hivyo kuwa mnyenyekevu!

Kuhusu anatazama wapi wakati amenyanyua mikono yake kwa ajili ya kuomba du´aa, anatakiwa kutazama mbele yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1620
  • Imechapishwa: 27/05/2018