Wapandikizwa waliopenyezwa katika safu kwa ajili ya kuipasua safu


Swali: Sisi tunatoka Uingereza na tunaona kumeenea fitina kubwa. Msingi wake inakuwa ni mizozo ilioko kati ya Mashaykh wawili. Baada ya hapo tunaona namna waislamu wanavyogawanyika makundi mawili; kundi limoja linakuwa na Shaykh huyu na kundi lingine linakuwa na Shaykh mwingine.

Jibu: Hili si jambo lilioko London peke yake. Hilo hata hapa kwetu lipo; mambo ya mipasuko na mgawanyiko na kila mmoja anamchapa mwenzake. Hii ni fitina. Tunamuomba Allaah awalinde waislamu kutokamana na hayo. Ni wajibu kwa wanafunzi kunasihiana, wapatane na wasameheane kati yao na wasaidizane juu ya wema na uchaji. Mpasuko huu unatokamana na shaytwaan na wasaidizi wa shaytwaan. Wako walinganizi wapotevu na watu waliopandikizwa ambao wanawachochea vijana juu ya mambo hayo na kuyaeneza kati yao ili kutokee yaliyotokea au mabaya zaidi. Ni wajibu kwa wanafunzi wanasihiane, wasaidizane na wapatane pindi kunatokea kufahamiana vibaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=GFnREhKtNnE&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 06/10/2018