Swali: Mimi ni imamu wa msikiti. Wakati mwingine wanakuja waombaji na kuwaomba watu. Je, niwazuie na kuwafanyia ukali katika hilo au niwaachie kwa ajili ya kitengo maalum kinachoshughulikia mambo hayo?

Jibu: Waache kwa ajili ya kitengo hicho maalum. Kwa sababu ukianza kuwazuia basi kutakuwa na vurugu msikitini. Pia jambo hili ni gumu kwako kwa sababu wewe sio askari msikitini. Kitengo maalum ndio kitawafatilia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 50
  • Imechapishwa: 08/06/2021