Miongoni mwa watu wako wanaowadarua wanachuoni na wanasema:

“Wao ni wanamme na sisi ni wanamme. Kwa nini mnawauliza wanachuoni na mnachukua maoni yao na wala hamtuulizi sisi? Wao ni wanamme na sisi ni ni wanamme.”

Hayo yanasemwa hii leo. Wale wanaojifanya kuwa ni wasomi na wajinga husema:

“Wao ni wanamme na sisi ni ni wanamme.”

Maneno haya yalisemwa na Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) katika wakati wake. Imaam Abu Haniyfah ni wa kwanza katika wale maimamu wanne. Aliishi katika zama za wanafunzi wa Maswahabah. Alichukua elimu yake kutoka kwa wanafunzi wa Maswahabah. Ni miongoni mwa watu walioishi katika zama bora. Bali imesemekana kuwa alikutana na alichukua elimu yake kutoka kwa Maswahabah. Kwa hiyo ima ni katika wanafunzi wa Maswahabah au ni katika wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah au ni katika wanafunzi wa Maswahabah. Yeye (Rahimahu Allaah) ndiye alisema:

“Inapokuja Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi tunaipokea kwa kuridhia. Inapokuja Hadiyth kutoka Maswahabah – bi maana Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – tunaipokea kwa kuridhia. Inapokuja kutoka kwa wanafunzi wa Maswahabah, basi wao ni wanamme na sisi ni wanamme.”

Ni marafiki. Wote walikuwa ni wanachuoni. Maana ya kwamba wao ni wanamme bi maana wanachuoni:

“Wao ni wanamme na sisi ni wanamme.”

Maneno haya yanasemwa na wajinga hii leo na watu wanaojifanya kuwa ni wasomi. Wanatoa fatwa. Wanapoambiwa kwamba ni kosa na ni jambo linakwenda kinyume na maoni ya wanachuoni wanaofuatwa na Ummah, ndipo husema:

“Wao ni wanamme na sisi ni wanamme.”

Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu! Unajilinganisha nafsi yako wewe na Abu Haniyfah, wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah na kusema kwamba:

“Wao ni wanamme na sisi ni wanamme.”

Hakika ipo tofauti kubwa sana! Ni lazima kwa mtu atambue nafasi ilionayo nafsi yake. Allaah amrehemu mtu ambaye ameitambua nafasi ilionayo nafsi yake. Ni lazima kwa watu wazindukane juu ya mambo haya na waiheshimu elimu na wanachuoni na wasiwadharau, ijapokuwa kutatokea makosa kutoka kwa baadhi yao. Kitabu cha Allaah na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee ndivo vimekingwa na kukosea. Kuhusu wanachuoni wanaweza kukosea. Lakini kupatia kwako ndio kwingi kuliko kukosea kwao. Jengine ni kwamba hawakukusudia makosa. Ni wenye kustahiki na wenye upeo. Mjinga anaweza kusema kwamba yeye pia hakukusudia kukosea na kwamba yeye pia anao upeo wa kufanya Ijtihaad. Tunamwambia kwamba yeye hastahiki na wala hana upeo wa kufanya Ijtihaad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/13252 Tarehe: 1432-04-05/2011-03-11
  • Imechapishwa: 07/06/2020