Swali: Ni kwa nini wafuasi wa Mitume mwanzoni mwa ulinganizi wao wanakuwa watu wanyonge?

Jibu: Kwa sababu watu madhaifu hawana kitu cha kuwazuia. Kuhusu wale wakuu, watukufu na matajiri ubwanyenye wao, vyakula vyao na matamanio yao huwazuia kufuata. Kwa ajili hiyo wale wanyonge wanakuwa wa mwanzo kuitikia.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watukufu na matajiri waliomfuata ni wachache. Mmoja wao ni Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh). Yeye ndiye wa kwanza aliyemwamini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 05/10/2018