Wanawake wasisahauliwe katika maudhui ya Khutbah

Wanawake wanatakiwa kutolewa nje katika swalah ya ´iyd, jambo ambalo tayari tumeshatangulia kulibainisha. Wanatakiwa kuelekezewa mawaidha maalum ndani ya Khutbah ya ´iyd. Kwa sababu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoona kuwa wanawake hawasikii, basi aliwaendea ambapo akawapa mawaidha na akawasisitiza juu ya kutoa swadaqah. Namna hii wanawake wanatakiwa wawe na sehemu katika maudhui ya Khutbah ya ´iyd kwa sababu ya kuhitajia jambo hilo na pia kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/276)
  • Imechapishwa: 29/07/2020