Wanawake wanapata fadhilah za mkusanyiko?

Swali: Sisi tuko zaidi ya wanawake sita ambao tunaishi katika nyumba moja. Nyakati za swalah za faradhi hupita na tunaswali kila mmoja kivyake. Tumejiwa na baadhi ya jamaa ambapo wakatunasihi kuswali swalah ya mkusanyiko na wakatubainishia kwamba kwa kufanya hivo tunapata fadhilah za mkusanyiko. Je, haya ni kweli?

Jibu: Wanawake hawana mkusanyiko. Lakini hakuna neno wakiswali mkusanyiko. Na kila mmoja akiswali peke yake hapana vibaya pia. Wakiswali mkusanyiko basi tunatumai kuwa wanapata fadhilah za mkusanyiko na khaswa ikiwa ni rahisi kwa mwanafunzi ambaye atawaongoza. Jengine ni kwa sababu kule kukusanyika kwao juu ya swalah kuna kusaidiana juu ya wema na kumcha Allaah. Imamu wao atasimama katikati yao katika safu ya kwanza na atasoma kwa sauti ya juu katika zile swalah za kusoma kwa sauti ya juu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/76)
  • Imechapishwa: 19/11/2021