Swali: Je, una nasaha zozote za kuwapa wanawake wanaokuja kuswali swalah ya Taraawiyh lakini hata hivyo wakati mwingine wanajitia manukato au wanavaa mavazi yasiyokuwa ya heshima?

Jibu: Nasaha zangu kwake aswali nyumbani kwake na hilo ni kheri na bora kwake. Si halali kwake kutoka nje hali ya kuwa amejitia manukato, kuonyesha mapambo, kutembea mwendo wa wanaume au akapiga kicheko na dada zake wengine masokoni. Kwani hakika hii ni sehemu khatari na fitina inashika kwenye mioyo kama moto kwenye mwitu.

Mosi namwambia kwamba kuswali kwake nyumbani ni bora kuliko kuswali kwake msikitini.

Pili ni kwamba akitoke nje basi atoke hali ya kujisitiri. Bi maana atoke pasi na kujitia manukato wala kuonyesha mapambo. Akitoke hali ya kujitia manukato basi atambue kuwa yuko katika khatari kubwa. Kwa hali hiyo atakuwa amemuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Mwanamke yeyote ambaye amepatwa na uvumba basi asishuhudie pamoja nasi swalah ya ´Ishaa.”

Hapa ni uvumba ambao [harufu yake] ni chini ya udi aina zengne.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1182
  • Imechapishwa: 16/05/2019