Wanawake wanaokwenda kuswali ´iyd wakionyeshe mapambo


Swali: Ni zipi nasaha zako juu ya wanawake wengi wenye kuonyesha mapambo wanapotoka kwenda kuswali swalah ya ´iyd?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Ni maovu. Ni lazima kuwazuia kufanya hivo. Wasijitie manukato, wasijipambe na wala wasionyeshe kitu. Wanatakiwa kutoka hali ya kujisitiri, hali ya kutojipamba, hali ya kutojitia manukato. Kwa sababu hii ni fitina. Akitoka hali hii hatafuti thawabu bali anachotafuta ni fitina. Kama kweli anatafuta thawabu basi anyenyekee, ajisitiri na hali ya kuwa na haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2019