Wanawake wafanye nini katika miji ambapo wamekataza Niqaab?


Swali: Ni ipi nasaha yako kwa yule mwenye kuishi katika mji ambapo wamekataza Niqaab na vipi mtu atataamiliana na kanuni hizi?

Jibu: Awahifadhi wanawake zake na ashikamane na Niqaab. Wao hawakatazi Niqaab isipokuwa kwenye vyuo vyao na sehemu zao (za hadharani) wanapokutana. Usiende sehemu kama hizi. Usiende kwenye vyuo vya makafiri na minasaba yao. Usiende sehemu zao kama mwanamke wa Kiislamu. Baki nyumbani na kwenye makazi yako na himdi zote ni za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-6-9.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014