Swali: Inasemekana kwamba ´Awrah ya mwanamke mbele ya mwanamke mwenzake ni kati ya kitovu na magoti…

Jibu: Hapana. Hili ni kosa. ´Awrah ya mwanamke mbele ya mwanamke mwenzake ni kama ´Awrah yake mbele ya Mahram zake wa kiume. Inajuzu kwake kumuonyesha baba yake au kaka yake kila kitu mbali na kilichoko kati ya kitovu na magoti? Hakuna mwanamke wa Kiislamu anayefanya hivo. Mwanamke akiwa na mwanamke mwenzake ni kama mwanamke aliye na Mahram zake wa kiume. Hivyo ndivyo alivyosema Allaah katika “an-Nuur”:

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ

“Waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazihifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao [dada zao wa Kiislamu].”[1]

Amewafanya wanawake ni kama wale Mahram zake wa kiume; haifai kwake akawaonyesha wanawake kitu isipokuwa yale anayowaonyesha Mahram zake wa kiume. Hakuna anayesema kuwa awaonyeshe Mahram zake miguu yake, kifua na mgongo. Hakuna yeyote anayesema hivo.

[1] 24:31

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 17/03/2017