Wanawake Kutokatoka Majumbani Mwao – Chanzo Cha Kupotea Kwa Haya

Swali: Kuna mwanamke anafunza Qur-aan msikitini na wakati mwingine inamjia hedhi yuko msikitini. Je, akiwa katika hali hiyo inafaa kwake kwenda kuwafunza dada zake Qur-aan msikitini?

Jibu: Hapana. Kwanza kitendo chake cha yeye kwenda kufunza msikitini kinatakiwa kuangaliwa vizuri. Anatakiwa kufunza nyumbani kwake. Kitendo cha mwanamke kwenda kufunza nje ya nyumba yake kimesababisha kupotea kwa haya na wanawake kuchukua usahali wa kutoka. Waje nyumbani kwake kujifunza kwake. Hili ni bora zaidi. Mwanamke asiende msikitini. Inahusu wale wanafunzi na mwalimu. Wasende hata mahala pa kuswalia (Muswallaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 20/11/2016