Wanawake kuswali mkusanyiko wakati wanapotoka kwenda mahali

Swali: Dada anauliza. Wanatoka na idadi ya ndugu. Wakati wa kuingia kwa swalah wanaswali mkusanyiko. Wanaswali swalah za kusoma kwa sauti na swalah za kusoma kwa siri sawa na kama wanavyoswali wanaume. Je hili ni katika mambo yanayojuzu?

Jibu: Hakuna neno wanawake wakaswali mkusanyiko. Lakini Imamu awe katikati yao na asiende mbele. Imamu wao awe katikati ya safu ya kwanza. Hakuna neno wakasoma kwa sauti katika swalah za kusoma kwa sauti ikiwa ni wanawake tu na hakuna wanaume, hakuna neno. Aswali kwa kusoma kwa sauti katika swalah za kusoma kwa sauti na aswali kwa kusoma kwa siri katika swalah za kusoma kwa siri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com//Live/ArID/528
  • Imechapishwa: 15/09/2020