Wanawake kupulizia udi na uvumba katika kumbi za harusi

Swali: Napenda kuuliza hukumu ya wanawake kufukiza uvumba katika majumba ya harusi wakati wa matamasha. Je, ni katika mambo yanayofaa Kishari´ah pamoja na kuzingatia kwamba imekuwa ni miongoni mwa desturi za watu wakati wa harusi zao. Wakati mwingine mwanamke anaweza kutoka pamoja na dereva au mwanaume ambaye si Mahram kwake.

Jibu: Hafai wakatumia haya. Wanawake wasitumie uvumba. Isipokuwa ikiwa kama atakupizia sehemu pasi na mwanamke kuchukua nguo zake na kuzipulizia. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote ambaye amepatwa na uvumba basi asishuhudie pamoja nasi swalah ya ´Ishaa.”

Hapa kunamaanishwa swalah zote. Lakini kwa mfano atapulizia uvumba huu sehemu maalum au katika safu mbalimbali bila mwanamke huyo kuchukua uvumba huo na kuanza kujipulizia mwenyewe, hakuna neno kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1242
  • Imechapishwa: 22/09/2019