Wanawake kupiga makofi katika sikukuu na sherehe

Swali: Je, inajuzu kwa wanawake kupiga makofi katika sikukuu za ndoa na sherehe ili kutangaza…

Jibu: Hapana. Haijuzu kupiga makofi. Ni kujifananisha na makafiri. Kinachojuzu ni wanawake kupiga makofi katika swalah pale ambapo imamu anasahau. Katika hali hiyo atamzindua imamu kwa kupiga makofi. Hili ndio lililothibiti kwa dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-25.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020