Swali: TV imekuwa ni njia ya kilimwengu na ya kiburudani ambapo kupitia njia hiyo zinaonekana picha za wanawake, wanaume, wanyama na vyenginevyo. Unasemaje kuhusu picha hizi zinazotikisika ambapo wanawake wanaonekana kwenye TV wakiwa na mapambo yao ya kawaida au wakiwa na Hijaab zao za Kiislamu kwa sauti zao zenye kuathiri.

Jibu: Kuonekana wanawake katika TV wakiwa ni wenye kuonyesha mapambo au wenye kuachia uso wazi haijuzu. Kuhusu wao kuonekana wakiwa wamevaa Hijaab na wakati huohuo wamejisitiri mwili mzima kukiwemo uso katika kuzungumza, kutoa nasaha na maelekezo au kueleza kuhusu kitu haidhuru. Kama ambavyo anavyozungumza katika vikao miongoni mwa vikao mbalimbali au mahali miongoni mwa mahali ya kwamba amefanya kitu fulani na mfano wa hayo.

Kuhusu kuonekana akiwa ni mwenye kuonyesha mapambo na uso wazi, haijuzu. Ni mamoja katika TV au kwenginepo. Hapa ni mbele ya wale wanaume ambao ni wageni kwake. Hili linahusiana hata nyumbani kwake au katika kikao chake. Haijuzu kwake kufanya hivo. Katika TV ndio shari zaidi kwa kuwa anaonekana na watu wengi ambao hawawezi kudhibitiwa idadi. Ni dhambi kubwa. Haijuzu kufanya hivo. Akiwa ni mwenye kuonyesha mapambo, amejitia vipodozi na mrembo basi dhambi yake inakuwa kubwa na mbaya zaidi. Vilevile fitina yake inakuwa kubwa zaidi. Vivyo hivyo inahusiana na mwanaume kama tulivyotangulia kusema akionekana katika TV na vile viungo visivyotakiwa kuonekana vikaonekana – kama hali inavyokuwa katika baadhi ya michezo ya kimazoezi – hili pia halijuzu. Haijalishi kitu hata kama ni mwanaume vikaonekana vile viungo visivyotakiwa kuonekana kama vile mapaja na vyenginevyo. Ni dhambi na haijuzu. Angalau kwa uchache anatakiwa kufunika vile viungo visivyotakiwa kuonekana ambapo ni baina ya kitovu na magoti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17784/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B8%D9%87%D9%88%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%84%D9%81%D8%A7%D8%B2
  • Imechapishwa: 07/10/2018