Swali: Una nini cha kuwaambia wale wamiliki wa nyukumbi za starehe na nyukumbi za harusi kutokana na yale yanayopatikana katika kunyanyua sauti za nyimbo kupitia vipaza sauti au wanakaa wanaume wanasikiliza nyimbo za watoto wa kike inayotoka kwa nje. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Maoni yangu ni kwamba kitendo hichi ni haramu sauti ya wanawake kusikika kwa wanaume ambao wanakaa, kuwasikiliza na wanastareheka kwa sauti zao. Jengine ni kwamba kufanya hivo kuna kuwaudhi majirani. Wajibu kwetu juu ya neema hii ni kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall) na furaha isitufanye tukamuasi Allaah.

Miongoni mwa maovu yanayohusiana na haya ni kwamba baadhi ya waume wapumbavu wanaingia kwenye mkusanyiko wa wanawake na wanakaa mahali pamoja na mke wake palipotengwa kwa juu ambapo mwanaume huyo akawa anamzungumzisha na wakati huohuo wanawake wakawa mbele yao na nyuso zao zikawa wazi. Hili halina shaka juu ya uharamu wake na kwamba haijuzu.

Mimi nashangazwa na familia ya mwanamke ni vipi watamwacha mume kuingia kwenye mkusanyiko wa wanawake? Je, hawaogopi kukawepo mwanamke katika wale wanawake ambaye ni mrembo kuliko huyo mke wake? Hili linawezekana au haliwezekani? Linawezekana. Akiwa ni mrembo kuliko mke wake basi hapana shaka kwamba shauku yake kwa mke wake itapungua. Mtu akimwona mwanamke mrembo na mzuri zaidi kuliko mke wake shauku kwa mke wake itapungua na furaha yake itageuka kuwa malalamiko. Kwa ajili hiyo nakataza hili. Mcheni Allaah, enyi waja wa Allaah na jiepusheni na ujinga huu.

Ndoa sio kitu cha ajabu ambacho hakitokei kwa mwaka isipokuwa mara moja. Kila usiku kuna watu wanaoana. Hakuna haja ya kusherehekea kiasi hichi ambacho kinamtoa mtu nje ya Sunnah. Ama kuhusu yale yanayoafikiana na Sunnah kama kwa mfano wanawake kupiga dufu kwa sauti zisizonyanyuliwa wala zisizoamsha matamanivu, haya hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1263
  • Imechapishwa: 03/10/2019