Wanawake kuimba nyimbo za wasanii harusini  

Swali: Baadhi ya harusi wanaimba nyimbo ambazo inasemekana zimechukuliwa kutoka kwa baadhi ya wanawake waimbaji. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Tuliashiria hilo katika maneno yetu na tukasema ya kwamba ni wajibu kujiepusha na nyimbo zinazoenda kinyume na maadili au kuimba nyimbo zinazoenda kinyume na maadili. Hata kama zitakuwa ni nyimbo safi lakini ikisemekana kuwa ni nyimbo zinazoenda kinyume na maadili, hakika sisi hatuonelei kujuzu kwake. Kwa sababu kujifananisha kunaathiri katika nyoyo. Huenda baadhi ya wanawake wakaingiwa kwenye nyoyo zao kuwapenda wanawake walioimba nyimbo hizi zinazoenda kinyume na maadili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020