Wanatumia vidonge vya kukata hedhi ili wasile Ramadhaan hata moja


Swali: Baadhi ya wanawake wanatumia vidonge katika mwezi wa Ramadhaan bila kusimamiza. Wanafanya hivo ili wasipate ada ya mwezi kwa lengo wasile siku hata moja ya Ramadhaan. Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Mimi sioni neno wa kufanya hivo ikiwa hayo hayawadhuru. Sijui ubaya wowote juu ya hilo. Kwa sababu wao katika hilo wana manufaa makubwa ambapo wanataka kufunga pamoja na wengine na wasilipe baada ya hapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/200-201)
  • Imechapishwa: 24/05/2018