Wanatuita “Madaakhilah” – lakini tunaendelea kutahadharisha vurugu na maandamano


Swali: Hapa Misri tunawashauri watu kutofanya maandamano, mapinduzi  na kuwafanyia uasi watawala. Baadhi ya watu wanatuita sisi kuwa ni “Madaakhilah” na “Jaamiyyah”.

Jibu: Hakuna tabu. Waache waseme. Hakukudhuruni kitu.

Swali: Unatunasihi nini?

Jibu: Endeleeni kutahadharisha fitina na shari. Mnalipwa thawabu Allaah akitaka.

Muulizaji: Wanatukana ulinganizi katika Sunnah kwa majina bandia kama haya “Madaakhilah” na “Jaamiyyah”.

Jibu: Hakuna tabu. Waache waseme. Hakukudhuruni kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=zwkNwp2g6ko
  • Imechapishwa: 15/11/2017