Wanatakiwa kufunga na kutoa chakula

Swali: Je, ni lazima kwa mjamzito na mnyonyeshaji kulipa funga zao wakila kwa sababu ya kuchelea kwao juu ya mtoto? Nimesikia baadhi ya ndugu wakisema kuwa si lazima kwao kufanya mambo hayo kwa sababu wanaingia chini ya maneno Yake (Ta´ala):

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

“Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga swawm] lakini kwa tabu watoe fidia kulisha masikini.”[1]

Jibu: Ni lazima kwao kulipa funga zao pamoja na kumlisha maskini kwa kila siku moja kwa sababu ya kuacha kufunga kwa sababu ya khofu ya mtoto. Msafiri na mwanamke mwenye hedhi pia ni lazima kwao kufunga pasi na kulisha.

[1] 02:184

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mufti.af.org.sa/ar/content/%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%A7%D9%85%D9%84-%D9%88%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%B6%D8%B9-%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B6%D8%A7%D8%A1-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A5%D8%B7%D8%B9%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 03/05/2020