Swali: Kuna baadhi ya waswidi ambao wanaona kwamba kueneza na kusambaza fataawaa za wanachuoni wetu kama zinazohusu Fiqh na mfumo zilizotolewa na mfano wa Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na al-Fawzaan kwamba ni upumbavu na ujinga na kwamba ni sababu ya kufarikiana kwa vijana. Unasemaje juu ya hilo pamoja na kuzingatia kwamba fataawaa hizo tayari ziko hadharani na zimeenea kati ya watu?

Jibu: Yule mwenye kutahadharisha dhidi ya watu hawa ni mtu wa Bid´ah na mpumbavu. Hakuna anayetahadharisha watu hawa isipokuwa mpumbavu na mtu wa Bid´ah. Sio katika Ahl-us-Sunnah. Hivyo amche Allaah juu ya nafsi yake na atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lau kama kweli angelikuwa ni Salafiy basi angelizisambaza na akawahimiza watu kuzieneza.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=w4wNkEV4HaY&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 10/02/2019