Wanaswali kwa kujificha kwa kuchelea wasije kuadhibiwa

Swali: Kuna watu wanaishi katika nchi za makafiri na wako katika shule ya bweni na hawawezi kuswali ndani ya wakati wake kwa kuchelea wasionekana na wakafukuzwa katika shule hiyo. Wafanye nini?

Jibu: Ikiwa waislamu wanaishi katika nchi ya makafiri na wanakhofia wakidhihirisha swalah zao wataadhibiwa basi inafaa kwao kuswali majumbani mwao au shuleni. Hakuna vibaya kwao kufanya hivo:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Lakini wakiwa wenye amani basi ni lazima kwao kudhihirisha swalah. Wasipojihisi amani basi waswali majumbani au katika shule yao mpaka Allaah atakapowasahilishia Hijrah na kuhamia nchi ya waislamu. Watapoweza kuhajiri kwenda katika nchi ambayo wataweza kudhihirisha dini yao basi itawalazimu kufanya hivo. Muda wa kuwa hawawezi wanalazimika kumcha Allaah. Wakishindwa kuswali waziwazi basi wataswali majumbani mwao na katika masomo yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4313/حكم-من-يخشى-اظهار-صلاته-في-بلد-كفر
  • Imechapishwa: 16/06/2022