Swali: Ni lipi bora kwa mswaliji kusimama nyuma ya imamu katika swalah yake au upande wa kuliani mwake?

Jibu: Akiwa peke yake basi asimame upande wa kuliani mwake. Wakiwa ni kundi zaidi ya mmoja basi wapange safu nyuma yake na wala asisimame yoyote upande wa kuliani mwake isipokuwa maeneo yakiwa pamejibana na asipate nafasi. Hivi ndivo Sunnah. Wanapaswa kuwa nyuma yake na kuliani mwake mahali pakiwa pamejibana. Kuliani mwake imamu ni bora kuliko kushotoni. Upande wa kulia mwa safu ni bora kuliko upande wake wa kushoto ijapo upande wa kushotoni mwake uko karibu zaidi na imamu. Kuhusu nyumani kwake ndio kuko karibu zaidi kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 18/09/2021