Wanaotoka katika maandamano ni wapenda fitina


Swali: Wale wanaotoka kwenda katika maandamano kisha wanauawa mtu awahukumu kuwa ni mashahidi kwa kuwa wametoka ili kutafuta haki zao?

Jibu: Je, wao wametoka katika njia ya Allaah mpaka waambiwe kuwa ni mashahidi? Anayetoka katika njia ya Allaah ndiye shahidi. Wewe unasema kuwa wametoka kwa ajili ya haki zao, bali wametoka kwa ajili ya tamaa za kidunia ikiwa kama kweli ni sahihi au wametoka kwa ajili ya fitina kwa ajili wanapenda fitina na ugomvi. Allaah ndiye Anajua zaidi nia zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (60) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mokh_2_1_1433.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014