Wanaostahiki Na Wasiostahiki Uongozi


Ni wajibu katika kuchagua viongozi na watawala kufuata mfumo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Uongozi huu hautakiwi kupewa yule ambaye anauomba, anaupupia au akajiweka katika wale wabunge wa kupigiwa kura, jambo ambalo ni katika kuupupia. Anatakiwa kuchaguliwa yule ambaye ana elimu, kuipa nyongo dunia na anamcha Allaah zaidi.

Jengine ni kwamba tunatakiwa kufaidika na mfumo huu wa utume inapokuja katika malezi. Hafai tukawalea vijana katika kupenda kuongoza, uraisi, ubwanyenye na utawala. Iwapo tutawalea juu ya kupenda mambo haya basi tutakuwa tumeenda kinyume na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na vilevile tutakuwa tumewatumbukiza vijana katika maangamivu. Tunatarajia kufaulu kupi duniani na Aakhirah iwapo tutaenda kinyume na mfumo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

وَيَقُولُونَ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالرَّسُولِ وَأَطَعْنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ وَإِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ

”Wanasema: “Tumemwamini Allaah na Mtume na tumetii” kisha hugeuka kundi miongoni mwao baada ya hayo na wala hao si wenye kuamini. Wanapoitwa kwa Allaah na Mtume Wake ili awahukumu baina yao mara hapo kundi miongoni mwao wanakengeuka.”[1]

[1] 24:47-48

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj-ul-Anbiyaa´ fiyd-Da´wah ilaa Allaah fiyhi al-Hikmah wal-´Aql, uk. 124
  • Imechapishwa: 19/02/2017