Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kwamba Allaah yuko kila mahali?

Jibu: Ni kufuru. Hivo ndivo wasemavyo Huluuliyyah. Wanaosema kwamba Allaah yuko kila mahali ni Huluuliyyah. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Allaah yuko juu ya viumbe Wake:

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

“Naye ni Mwenye kudhibiti hali ya kuwa juu ya waja Wake.”[1]

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.”[2]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) yuko juu. Mwenye kusema kwamba yuko kila sehemu ni Huluuliy – na ni kufuru.

[1] 06:18

[2] 67:16-17

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (80) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-17-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 26/11/2018