Wanaopinga Allaah kuwa juu wanaingia katika moja ya kauli hizi

Ni lazima kubainisha madhehebu yao ili yasiwahadae baadhi ya watu. Wakati walipopinga kuwa Allaah hakutengana na viumbe Vyake na kwamba hayuko juu, wakawa wameingia katika mambo matatu:

1- Jambo la kwanza ni kusema wazi kuwa Allaah hayupo. Hawakuchagua hili kwa kuwa [Malaahidah] walijua kuwa watu watawaumbua na kufuru yao.

2- Jambo la pili ni kusema kuwa Allaah hayuko ndani ya ulimwengu, nje ya ulimwengu, juu wala chini, hakufungamana nao na wala hakutengana nao kama walivosema hilo Jahmiyyah ambao wamemkanusha Allaah kwa kukusanya mambo mawili yanayojigonga. Hakuchagua hili [Ibnul-´Arabiy] kwa sababu alionelea kuwa haliingii akilini.

3- Akachagua kauli ya tatu inayosema kuwa Allaah ni sehemu ya viumbe hivi. Kila unachokiona ndio mola. Namna hii ndivyo alivosema Ibnul-´Arabiy…

Hawa ni makafiri. Hawaamini kuwepo kwa Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Aakhirah, Qadar; kheri na shari yake. Hawa ndio makafiri wabaya zaidi.

Miongoni mwa athari za madhehebu haya wanasema kuwa Fir´awn alipatia pindi aliposema:

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Akasema: “Mimi ni mola wenu mkuu.” (79:24)

Kadhalika waabudu masanamu na mizimu wako katika haki na usawa. Vilevile kila mwenye kuabudu kitu ni mwenye kupatia. Mwenye kuabudu moto amepatia. Mwenye kuabudu sanamu amepatia. Mwenye kuabudu ndama amepatia. Wanaonelea kuwa kufuru ni kule mtu kulenga. Wanaonelea kuwa usimkataze yeyote na kuabudu kitu. Ukikhusisha kitu na kusema haijuzu kuabudu vitu hivi, basi hii ndio kufuru kwa mujibu wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/158-159)
  • Imechapishwa: 30/05/2020