Wanaolipwa na wasiolipwa wakati wa kufanya jimaa   

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

25- Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Baadhi ya Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ee Mtume wa Allaah! Wenye mali wameondoka na fungu kubwa; wanaswali kama sisi, wanafunga kama sisi na wanatoa swadaqah ya ziada ya mali zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah hajakufanyieni vitu kwa ajili yenu kutoa swadaqah? Hakika kila Kusema “Subhana Allah” ni swadaqah, kusema “Allahu Akbar” ni swadaqah, kusema “Alhamduli Allaah” ni swadaqah, kusema “Laa ilaaha illa Allaah” ni swadaqah, kulingania jambo jema ni swadaqah, kukataza maovu ni swadaqah na katika kujamii [wake zenu] kila mmoja katika nyinyi ni swadaqah. Wakasema: “Ee Mtume! Mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake? Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mnadhani ingekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu angelipata dhambi? Na hivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.”

Ameipokea Muslim.

Wanachuoni wametofautiana juu ya masuala haya. Je, mtu mwanaume anapewa ujira kwa kuiendea halali pasina kunuia hilo au anapewa kwa kule kuiendelea halali kwa kunuia?

1- Kundi la kwanza: Shahawa hizi ambazo Allaah Amempa mtihani kwazo mja, akiziweka [shahawa zake] katika halali [mkewe] analipwa ujira kwa hilo bila ya nia kama ilivo udhahiri wa Hadiyth hii. Nia ya ujumla ambayo ni ya utiifu na ya Uislamu itamnufaisha. Anapewa ujira kutokana na nia ya Uislamu na ya kumtii Allaah (Jalla wa ´Alaa) kutokana na yale anayofanya na anayojiepusha.

2- Kundi la pili: Hadiyth hii inapelekwa katika Hadiyth nyinginezo ambazo zinasema kuwa atapewa ujira pale ambapo akijiepusha na haramu na kuiendea halali kwa kunuia hilo. Akijiepusha na kutumbukia kwenye zinaa na kuiendea halali kwa kunuia hilo, basi anapewa ujira kwa hilo. Kwa sababu Hadiyth nyingine, kanuni za jumla na vilevile baadhi ya Aayah zinaonyesha ya kwamba anapewa ujira kwa yale anayokusudia kwayo Uso wa Allaah (Jalla wa ´Alaa)…

Wanachuoni wengi wameichukulia Hadiyth kama jinsi yalivo maandiko mengine ambayo yanasema kuwa mja analipwa ikiwa ataiendea halali na kujiepusha na haramu kwa kunuia hilo. Akinuia ndani ya moyo wake kuwa hatofanya haramu kwa kuwa Allaah Amemhalalishia halali na hivyo anakomeka tu na halali bila ya haramu, basi anapewa ujira kwa nia hiyo. Hakika ya kila ´amali inategemea na nia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 363-364