Wanaoishi au kutembea karibu na msikiti kuongea wakati wa Khutbah ya ijumaa


Swali: Nikiwa naishi karibu na msikiti na namsikia Khatwiyb siku ya ijumaa akitoa Khutbah na mimi huku niko nyumbani namzungumzisha mke wangu au watoto wangu ilihali imamu anakhutubu au kwa mfano nikawa karibu na msikiti barabarani natembea nikamtolea salamu ambaye yuko pembeni yangu na yeye akaitika salamu yangu. Je, tunaguswa na Hadiyth:

“Mwenye kufanya upuuzi basi hana ijumaa.”?

Je, nirudi swalah yangu?

Jibu: Kuhusu kurudi swalah hakuna kuirudi. Hata kama mtu atazungumza katikati ya msikiti na huku imamu anatoa Khutbah, swalah yake ni sahihi. Lakini hata hivyo ni mwenye kunyimwa thawabu. Kwa msemo mwingine ni kwamba haandikiwi thawabu za yule aliyenyamaza na hakuzungumza.

Kuhusu kuongea kwake na mke wake nje ya msikiti au njiani, ikiwa anasikia Khutbah ya yule imamu ambaye anataka kuswali nyuma yake, basi atambue kuwa haifai kwake kufanya hivo. Kwa sababu huyu ni imamu wake. Ama ikiwa Khutbah anayosikia ni ya imamu wa msikiti mwingine kwa njia ya kwamba huku anatembea na akamsikia yuko anakhutubu, hakuna ubaya kwake akazungumza wala hilo halimdhuru. Ni mamoja akaongea na mke wake au njiani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/835
  • Imechapishwa: 25/03/2018