Wanaofanya uasi dhidi ya watawala wa Kiislamu ni katika Ahl-us-Sunnah?


Wale ambao wanaomba dhidi ya watawala wa Waislamu sio katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kadhalika wale wasiowaombea. Hii ni alama ya kwamba yuko na upindaji katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Baadhi ya watu wanawakataza wale wenye kuwaombea watawala katika Khutbah na wanasema kuwa huku ni kuwapaka mafuta na unafiki. Ametakasika Allaah! Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Bali katika Sunnah ni kuwaombea du´aa watawala. Kwa sababu wakinyooka na watu pia watanyooka. Wewe unachotakiwa ni kuwaombea wema na uongofu na kheri hata kama wana mabaya. Lakini vilevile wana mazuri. Maadamu bado ni waislamu wana kheri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah, Uk. 172
  • Imechapishwa: 05/09/2020